Featured Posts
Sunday, September 21, 2014
Saturday, June 21, 2014
Maandalizi ya Mwisho Kili Tour Iringa,Usikose Mkazi wa Iringa
Wakazi wa Iringa wanatarajia kushuhudia wanamuziki zaidi ya 10
wakipanda jukwaani katika Kilimanjaro Music Tour 2014 ambayo itafanyika
uwanja wa Samora. Kuelekea show hiyo maandalizi ya mwisho yameendelea
ambapo majukwaa ndani ya uwanja na mabanda yalikuwa yakijengwa.
Hizi ni baadhi ya picha toka uwanja wa Samora.
Muonekano wa geti la kuingilia uwanja wa Samora
Muonekano wa jukwaa toka kwa pembeni ya uwanja
Muonekano wa jukwaa kwa upande wa nyuma ya jukwaa
Ufungaji wa taa za juu ya jukwaa
Eneo litakalotumika kwa ajili ya kugawa Kilimanjaro Premium Lager ya bure kwa mashabiki watakaojitokeza
Hizi ni baadhi ya picha toka uwanja wa Samora.
Muonekano wa geti la kuingilia uwanja wa Samora
Muonekano wa jukwaa toka kwa pembeni ya uwanja
Muonekano wa jukwaa kwa upande wa nyuma ya jukwaa
Ufungaji wa taa za juu ya jukwaa
Eneo litakalotumika kwa ajili ya kugawa Kilimanjaro Premium Lager ya bure kwa mashabiki watakaojitokeza
Thursday, June 12, 2014
MISS IRINGA KUFANYIKA JUNE 20
Baadhi ya washiriki wa redds miss iringa wakiwa katika picha ya pamoja kabla ya mazoezi katika ukumbi wanakofanyia mazoezi hotel ya Gentle Hill iliyoko mkoani Iringa.
Na Denis Mlowe,Iringa
HATIMAYE kinyang’anyiro cha kumsaka Redds Miss Iringa kinatarajia kufanyika Juni 20 mwaka huu baada ya aliyekuwa mratibu wa kwanza Mohamed Mcholeka kutoweka katika mazingira ya kutatanisha na kushindwa kufanyika Juni 6 kama lilivyopangwa mwanzoni na Tanzania Daima kuwa la kwanza kuripoti kuhusiana kutoweka kwa shindano hilo.
Waandaji wa Redds Miss Tanzania chini ya Lino Agency Hashim Lundenga baaada ya kugundua hilo wamempatia kibali cha kuandaa shindano hilo ambalo lilikuwa linasubiriwa kwa hamu kubwa na wadau wa tasnia ya urembo na kwasasa Redds Miss Iringa imepata mratibu mwingine ambaye ni kutoka kampuni ya Chakudika Intertainment chini uongozi wake Victor Chakudika ambaye ni Meneja wa kituo cha radio ya Nuru Fm ya mjini Iringa.
Akizungumza na Tanzania Daima ofisini kwake jana Mkurugenz wa kampuni hiyo, Victor Chakudika alisema maamuzi ya kuandaa shindano la Redds Miss Iringa kwa lengo a kutopoteza vipaji vya mabinti waliokuwa tayari kushiriki shindano hilo na kuondoa aibu ya mkoa wa Iringa kutopelekwa mwakilishi katika shindano la Redds Nyanda za Juu ambako wamekuwa wakishiriki kila mwaka.
Alisema kuwa shindano la Redds Miss Iringa limekuwa chachu ya ajira kwa mabinti wengi mkoani hapa kwa kuweza kutangaza vipaji vya washiriki wanaojitokeza kushiriki kila mwaka.
Chakudika alisema shindano hilo linatarajia kuwa la kisasa kutokana na maandalizi yake kuendelea vyema na kuwataka wadau wa tasnia ya urembo ujitokeza kwa wingi katika ukumbi wa St. Dominic likalofanyika shindano hilo.
“Kwa kweli baada ya mratibu wa kwanza kukimbia kutokana na gharama za uandaaji niliamua kuchukua jukumu hilo kulikomboa shindano hilo lifanyike na warembo wengi wamejitokeza kushiriki miss iringa” alisema Chakudika.
Aliongeza kuwa hadi sasa warembo 12 wamejitokeza kushiriki shindano hilo na wanaendelea na mazoezi katika ukumbi wa Hotel ya Gentle hill ya mjini hapa. Aidha msanii Mo Music anayetamba na wimbo wake wa ‘Basi Nenda’ anatarajia kutoa burudani kali katika shindano hilo ,wasanii wengine chupukizi wa mjini Iringa, vikundi vya sanaa, Wakali wa Kudance wa mjini Iringa.
Aliwataja wadhamini wa shindano hilo licha ya TBL kupitia kinywaji chake cha Redds, wengine ni Nuru Fm, kampuni mpya ya mabasi ya Sutco High Class, Gentle Hills na kuwataka wadau zaidi kujitokeza kudhamini shindano hilo.
Tuesday, April 29, 2014
FURSA: MAFUNZO YA KUPIGA ALA ZA MUZIKI KUANZA TENA MWEZI MEI
Baadhi ya wanafunzi wakiwa kwenye mazoezi
Action Music Tanzania (AMTz) inatangaza fursa kwa watu wote kujiunga na mafunzo ya kupiga ala za muziki yanayoanza tarehe 3/5/2014, lengo likiwa ni kuwajengea uwezo wanamuziki wa kupiga ala na kufanya maonesho kwa weledi na utaalamu zaidi.
Baadhi ya wanafunzi wakiwa darasani
Mafunzo yanayotolewa ni pamoja na upigaji wa ala za muziki zikiwemo gita, kinanda, tarumbeta, saxophone, konga, drum set, na upigaji wa ngoma za asili. Pia yatatolewa mafunzo ya ‘body percussion’ yaani matumizi ya mwili katika kutengeneza midundo ya muziki.
Mafunzo hayo yanafanyika kwenye ofisi za AMTZ zilizopo maeneo ya Mwenge mtaa wa Umoja, nyuma ya magorofa ya jeshi na kwenye Idara ya Sanaa na Sanaa za Maonesho Chuo Kikuu cha Dar es Salaam ambapo ili kujiunga na mafunzo haya wasiliana nao kwa simu namba 0686928828/0653075791 ili kupata fomu za kujiunga na mafunzo.
Monday, April 7, 2014
PICHA ZA NEY WA MITEGO ALIPOFANYA MAHOJIANO NA UPLAND FM IRINGA
Mwaka ze Bwoy Kushoto,Ney wa Mitego na Franky Vegullah Vijana Toka UPLANDS FM Njombe Muda Mfupi baada ya Live Interview Usiku wa Jana Njombe.
PhD Franky Vegullah Akiwa na Nay wa Mitego
Mzee wa Makablasha Geble Gabriel Elias Kilamlya Akiwa na ze True Boy In Ze Building................Usiulize!!!!!!!!!!!!!!!!!
CHANZO:gabrielkilamlya
Saturday, December 28, 2013
Tuesday, November 12, 2013
CLUB TWISTER INAVYOZIDI KUTESA KWA KULETA WASANII MASHUHURI
hapa kama sio aifora basi ni mama halima
umati wa mashabiki uliojitokeza katika tamasha hilo
hapa akijiachia na shabiki wake
Subscribe to:
Posts (Atom)